DKT. BITEKO AZINDUA ZAHANATI YA BUNGONI - ILALA

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko leo tarehe 29 Disemba, 2023 amezindua Zahanati ya Bungoni iliyopo mtaa wa Mafuriko Ilala jijini Dar es Salaam na kuwataka wananchi kutumia fursa ya uwepo wa huduma ya zahanati hiyo kutumia huduma badala ya kwenda mbali kufuata huduma za Afya, kwani ni dhamira ya Serikali kusogeza huduma kwa wananchi. "Niwaombe viongozi wenzangu tuliopewa dhamana na Mhe. Rais kuhakikisha tunawahudumia kwa vitendo wananchi na kuinua hali za wanyonge kwa kuwapatia huduma bora wanazostahili." Alisisitiza Dkt. Biteko Aliwataka wananchi wa Ilala kumpa ushirikiano Mbunge wao kwa vitendo na kumpongeza kwa kazi kubwa aliyofanya ya kuleta Maendeleo kwa wanachi wake, na kuwataka viongozi wengine kuiga mfano wa Mbunge huyo kufanikisha ujenzi wa zahanati hiyo na kukemea wachache wanaojificha kwenye kivuli cha taratibu kuchelewesha maendeleo. Ujenzi wa zahanati hiyo ulianza mwezi februari mwaka huu, kwa jitihada za wananchi na baadae...