
CHANGAMOTO YA UHABA WA MAJI WATOWEKA SHULENI Moja ya changamoto zinazowakabili wanafunzi wengi wakiwa katika mazingira ya shule zao hapa nchini ni ukosefu wa huduma ya maji safi na salama kwa ajili ya matumizi ya usafi ,kupikia na kunywa. Hali hiyo huwasababishia magonjwa mbalimbali yakiwemo ya kuhara,minyoo na amiba na wakati mwingine hulazimika kutumia muda wa masomo kutafuta huduma ya maji na hata wanapoyafikia yanakuwa si safi na salama. Waumini wa kanisa la Pentekost Galilaya Tanzania lenye makau makuu yake katika mji wa Runzewe limeguswa na adha ya maji inayowakabili wanafunzi wa shule ya sekondari Siloka halmashauri ya wilaya ya Bukombe mkoani Geita baada ya kuvuta huduma ya maji safi na salama hadi shuleni hapo. Ilikuwa mapema ya February 13,mwaka huu waumini wa kanisa hilo walipokusanyika kwenye shule hiyo na kuchimba mtalo wa kupitisha bomba la maji hadi kuhakikisha maji hayo yanatoka katika shule hiyo. Akizungumziahatua hiyo kwa niaba ya Askofu mkuu wa kanisa hilo...